25 Oktoba 2016 - 20:38
Washirika wa Marekani wajadili hatima ya mapambano dhidi ya Daesh

Hofu na Mashaka yametanda kwa Marekani na washirika wake, walijiunga kwa madai ya kupambana na magaidi wa Daesh nchini Iraq na Syria, baada ya magaidi hao kuangamizwa kwa Juhudi za Majeshi ya Iran na Urusi, huku muungano huo ukiwasaidia magaidi hao badala ya kuwashambulia.

Shirika la habari la ABNA linaripti kuwa: Hofu na Mashaka yametanda kwa Marekani na washirika wake, walijiunga kwa madai ya kupambana na magaidi wa Daesh nchini Iraq na Syria, baada ya magaidi hao kuangamizwa  kwa Juhudi za Majeshi ya Iran na Urusi, huku muungano huo ukiwasaidia magaidi hao badala ya kuwashambulia.

 Mapambano yanaendelea dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh katika mji wa  Mosul nchini Iraq wakati mawaziri wa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh ukijadiliana juu ya hatma ya vita hivyo.

Katika wakati vikosi vya Iraq vikiongozwa na wataalamu wa vita kutoka Iran vikiendelea na mashambulizi mashariki mwa mji wa Mosul kuukomboa mji huo kutoka mikononi mwa kundi la kigaidi la Daesh linalojiita Dola la Kiislamu, mawaziri wa ulinzi kutoka nchi za muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani kupambana na kundi hilo wanakutana mjini Paris, Ufaransa, kutathimini operesheni yao hiyo ambayo haijaonyesha mafanikio yeyote. Mkutano huo wa Paris unafanyika huku kukiweko hofu na mvutano kati ya serikali ya Iraq na Uturuki ambayo imekuwa ikiwasaidia magaidi.

Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wameingiwa na mashaka baada ya majeshi ya Marekani kufungua njia ili magaidi waweze kukimbia katika mji wa Mosul Iraq, jambo lilipolekea magaidi wanaokadiriwa kufikia 500 kukimbia Iraq na kuelekea Syria ambapo kwa bahati nzuri walikushambuliwa vikali na ndege za kivita za Urusi, jambo lililoikasirisha sana Marekani ambayo ilitaka magaidi hao wakimbilie Syria na kuendeleza mapambo dhidi ya wananchi na serikali ya Syria.  Akizungumza katika mkutano huo wa mawaziri wa ulinzi, Rais Francoise Hollande wa Ufaransa amezitaka nchi zilizopo katika muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani katika kukabiliana na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh mjini Mosul, kujiandaa kukabiliana pia na matokeo yatakayosababishwa na kuporomoka kwa mji huo, ikiwa ni pamoja na kurudi tena kwa wapiganaji hao wa kundi la kigaidi la Daesh katika nchi zao ikiwemo nchi za Ulaya.

Hollande amesema hatua ya kuutwaa tena mji huo haijamalizika, kwa hivyo kila mmoja anabidi kutarajia athari zitakazosababishwa na operesheni yao. Tahadhari aliyoitowa Hollande inahusu pia kuanza kushuhudiwa wapiganaji wa kigeni wa jihadi wakirudi nyumbani kwao wakitokea eneo hilo la mapambano.

Maafisa wa ngazi za juu ya Iraq na Marekani wanasema tayari viongozi wa kundi la kigaidi la Daesh wameanza kujaribu kuukimbia mji huo na kuelekea Syria upande wa eneo wanalolidhibiti baada ya Marekani kuwafungulia njia.

Katika mapambano yanayoendelea, inaarifiwa kwamba vikosi maalum vya kijeshi vimekuwa vikijikusanya karibu na medani ya mapambano kufungulia njia mashambulizi ya nchi za Magharibi ambayo wanasema yanalenga kuutwaa tena mji wa Tal Afar na kuzifunga njia za kuelekea nchi jirani ya Syria zinazotumiwa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh wanaotoroka Mosul.

Vikosi  maalum vya jeshi la kupambana na ugaidi, CTS, viliyadhibiti tena maeneo ya karibu na vitongoji  vya mashariki mwa Mosul, maeneo ambayo ni ngome za mwisho za kundi la kigaidi la Daesh nchini Iraq.

Wakati huo huo, kundi la muungano wa kijeshi linalofahamika kama Hashed al-Shaabi ambalo linahodhiwa na wapiganaji mahiri wa Kishia kutoka Iran linajiandaa kwa upande wake kushambulia eneo la magharibi mwa mji huo wa Mosul, ingawa Marekani imepinga uwepo wa majeshi hayo yanayodhaminiwa na Iran ambayo yamesabisha ushindi mkubwa katika mapambano dhidi ya magaidi.

Marekani imeendelea kuchochea tofauti za kimadhehebu na ukabila ili kuleta tofauti katika safu za majeshi ya Iraq ili kuzidhoofisha katika mapambano dhidi ya magaidi lakini wairaq wengi wameipuuza marekani na kutanguliza maslahi ya nchi yao kwanza.

Hata hivyo, licha ya muungano wa kijeshi kukutana jijini Paris hivi leo, si Iraq wala Uturuki zinazohudhuria mkutano huo, huku pakitajwa tafauti kubwa ya kimkakati iliyopo kati ya majirani hao mahasimu kwenye vita dhidi ya magaidi, ambapo Uturuki inasaidia magaidi wa Daesh nchini Iraq na Syria.

Mawaziri wa ulinzi wanaokutana, wakiwemo mwenyeji Jean Yves Le Drian wa Ufaransa na mwenzake wa Marekani, Ashton Carter, watajaribu kuzitafutia ufumbuzi tafauti zao kuhusiana na vipaumbele katika operesheni hiyo pamoja na kutathmini vita hivyo dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh baada ya zaidi ya miaka miwili ya kuanzishwa mashambulizi ya angani ya vikosi vya muungano wa kijeshi ukiongozwa na Marekani ambao haukuonyesha mafanikio zaidi ya kuwasaidia magaidi na kushambulia vikosi vya Iraq na Syria na kisha kuomba radhi.

Mwisho wa habari/ 291